Na Mwandishi Wetu
UMOJA wa Wafanyabiashara wa Kariakoo jijini
Dar es Salaam, wameitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusu vibali vya Wachina
wanaofanya biashara za kimachinga baadala ya uwekezaji mkubwa.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa
Umoja huo, Peter Kyando wakati alipokuwa akizungumza na kuhusu muingiliano
huo wa biashara.
Alisema umoja huo unaitaka serikali kufanya
hivyo kutokana na wachina hao kuingilia biashara ambazo zingeweza kufanywa na
Wafanyabiashara wadogo wa Tanzania, anaamini vibali vyao haviwaruhusu kufanya
hivyo.
Kyando alisema ingawa ni kweli
wafanyabiashara wa hapa nyumbani wanalalamikia Wachina hao lakini bado
wanaowajibika kutoa taarifa zao ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Viwanda
na Biashara ambazo zinajua taarifa za vibali vya uingiaji wa watu hao.
Aliongeza kuwa baadhi ya wafanyabiashara
wanahoji iwapo serikali imewaruhusu Wachina hao kufanyabiashara hizo baadala ya
kukaa kimya.
Kyando alisema inasikitisha kuwaona wachina
waliodhaniwa kuwa ni wawekezaji wakubwa wakiuza barafu, maua, sufuria, mifuko
ya kike na simu kwa mtindo wa kimachinga.
Kyando alisema yote hayo yanafahamika na
wizara husika lakini kwa sababu malalamiko hayo yalikwisha wafikia na isitoshe
hata watendaji wake wakipita maeneo ya Kariakoo wanajione lakini cha kushangaza
wizara hizo zimekaa kimya.
“Unajua serikali yetu nayo inawakatisha tamaa
wananchi wake kwa sababu wanajua kinacho lalamikiwa laikini wamekaa kimya sasa
labda wanagoja wananchi wandamane”alisema Kyando.
Aidha, Kyando alisema ni jambo la ajabu
kuwaona Wachina hao wakifanya wanavyotaka wakati Watanzania wanapokwenda China
wanaulizwa maswali kuwa kilichowapeleka huko pia hawaruhusiwi kuendesha
biashara ambazo wanaweza kuzifanya wenyeji wa huko.
Ni hivi karibuni wananchi mkoani Dodoma na
Pwani walishangaa kuwaona wamachinga wa kichina waliokuwa wakipita kila
mgahawa, baa na kwenye mikusanyiko ya watu wakiuza simu za viganjani.
No comments:
Post a Comment